1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kallas: Machafuko dhidi ya waandamanaji wa Iran hayakubaliki

Josephat Charo
9 Januari 2026

Umoja wa Ulaya unasema machafuko dhidi ya waandamanaji wa Iran hayakubaliki.

https://p.dw.com/p/56bKM
Kaja Kallas amesema ukandamizaji wa maandamano ya Iran na kutumia machafuko dhidi ya waandamanaji hakukubaliki.
Kaja Kallas amesema ukandamizaji wa maandamano ya Iran na kutumia machafuko dhidi ya waandamanaji hakukubaliki.Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema Ijumaa kwamba hatua zinazochukuliwa na vyombo vya usalama vya Iran kuyazima maandamano zimechupa mipaka.

Ameongeza kusema machafuko yoyote dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani hazikubaliki.

Kallas ameandika katika mtandao wa X akisema kufunga mtandao wa intaneti na kukandamiza maandamano kunaufichua utawala unaoogopa watu wake wenyewe.