1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kusuluhisha mzozo wa Ghuba

Oumilkheir Hamidou
15 Juni 2017

Licha ya lawama za rais Donald Trump, Marekani inaonyesha dalili za kutoiacha mkono Qatar mnamo wakati ambapo juhudi za kidiplomasia zimeshika kasi kuupatia ufumbuzi mzozo wa Ghuba.

https://p.dw.com/p/2ejx9
USA  Jim Mattis Qatar
Picha: picture alliance/Zumapress

 

Manuari mbili za Marekani zimetia nanga katika bandari ya Hamad kusini mwa mji mkuu wa Qatar Doha, ili kushiriki katika luteka pamoja na jeshi la wanamaji la Qatar-wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema.

Sambamba na hayo wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon imesema waziri wa ulinzi Jim Mattis na waziri mwenzake wa Qatar Khaled Al Attiyah wametiliana saini makubaliano ya kuuziwa Qatar ndege za kiita chapa F-15.

"Biashara ya ndege hizo ya dala bilioni 12 itaipatia Qatar teknolojia ya kisasa na kumarisha ushirikiano katika sekta ya usalama kati ya Marekani na Qatar, wizara ya ulinzi imesema.

Ushirikiano huo ni wa hali ya juu kwasababu Marekani tayari ina kituo cha jeshi la wanaanga katika jangwa la Qatar, yanakokutikansa pia makao makuu ya uongozi jumla wa kijeshi wa Marekani unaosimamia opereshini za kijeshi dhidi ya wafuasi wa dola la kiislam nchini Syria na Iraq.

Rais Donald Trump wa Marekani na mawaziri wake wa mambo ya nchi za nje Rex Tillerson (kushoto) na wa ulinzi James Mattis (kulia)
Rais Donald Trump wa Marekani na mawaziri wake wa mambo ya nchi za nje Rex Tillerson (kushoto) na wa ulinzi James Mattis (kulia)Picha: Reuters/K. Lamarque

Marekani inauma na kupuliza Qatar

Taarifa hizo zimetolewa siku kumi tangu uliporipuka mzozo wa kidiplomasia kati ya Qatar na Saud Arabia na washirikia wake. Nchi hizo zimevunja uhusiano wa kidiplomasia na Qatar inayotuhumiwa kuyaunga mkono mashirika ya itikadi kali, na kuwa karibu zaidi na Iran, hasimu mkubwa wa falme hizo za kiarabu katika Ghuba.

Mattis na Al Attiyeh wametilia mkazo umuhimu wa kumaliza mivutano ili washirika wote wa eneo hilo waweze kujishughulisha na awamu mpya ili kuyafikia malengo yao" hayo lakini ni kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya ulinzi ya Marekani.

Tangu mzozo ulipoanza, serikali ya mjini Washington imekuwa ikiuma na kupuliza. Katika wakati ambapo rais Trump anaonyesha kuunga mkono kutengwa Qatar, anayoituhumu "kugharaama ugaidi", wizara ya mambo ya nchi za njje na ile ya ulinzi Pentagone wanazidisha miito ya kutuliza hali ya mambo na kuhimiza majadiliano.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu (kushoto) na waziri mwenzake wa Qatar Abulrahman Al Sani
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu (kushoto) na waziri mwenzake wa Qatar Abulrahman Al SaniPicha: picture alliance/abaca/C. Ozdel

Juhudi za kidiplomasia zimeshika kasi

Juhudi za kidiplomasia zimeshika kasi kuupatia ufumbuzi mzozo huo uliopelekea mipaka tangu ya angani, nchi kavu na baharini ya Qatar kufungwa. Mbali na Marekani, Uturuki, Kuweit na Ufaransa pia wameingia mbioni . Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki Mevlut Cavusogli alikuwa ziarani  Qatar jana na leo hii anakwenda Kuweit kabla ya kwenda Saud Arabia kesho ijumaa kukutana na mfalme Salman.

Rais Recep Tayyip Erdogan anapanga kuzungumza kwa simu na rais Trump wa Marekani hivi karibuni. Msemaji wa ikulu ya Uturuki amesema pia kuhusu kuitishwa mazungumzo ya pande tatu kati ya viongozi wa Ankara, Paris na Doha mjini Ankara. Nae rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amepangiwa kukutana na kiongozi wa Falme za nchi za kiarabu . Zaidi ya hayo Kuweit pia inaendesha juhudi za upatanishi.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP/AFP

Mhariri:Josephat Charo