1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ukraine lavuka na kuingia katika jimbo la Kherson

18 Agosti 2023

Majeshi ya Ukraine yamevuka na kuingia katika ukingo wa mashariki wa jimbo la Kherson Ijumaa na kujiweka tayari kwa mapambano, haya ni kulingana na gavana wa Urusi katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4VJgr
Picha ya maktaba- Wanajeshi wa Ukraine wakielekea uwanja wa mapambano Kherson Novemba 18, 2022.
Picha ya maktaba- Wanajeshi wa Ukraine wakielekea uwanja wa mapambano Kherson Novemba 18, 2022.Picha: Bulent Kilic/AFP

Vladimir Saldo amesema wanajeshi hao walikuwa wamejificha nje kidogo ya mji unaodhibitiwa na Urusi wa Kozachi Lageri, karibu na mto Dnipro. Saldo anasema wanajeshi hao baadae walifukuzwa na majeshi ya Urusi.

Kauli ya Saldo inajiri baada ya waziri wa ulinzi wa Ukraine Ganna Malyar wiki hii kuthibitisha kwamba baadhi ya wanajeshi wa Ukraine walifanya majukumu kadhaa katika ukingo wa kushoto wa mto Dnipro huko Kherson.

Wakati huo huo Marekani imeidhinisha Uholanzi kuipelekea Ukraine ndege za kivita chapa F-16.

Haya yamesemwa na waziri wa ulinzi wa Uholanzi Kajsa Ollongren katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa X.

Ndege hizo lakini hazitoinufaisha Ukraine kwa sasa kwa kuwa majeshi yake yanahitaji kupewa mafunzo ya kuzitumia kwanza.