1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lauwa wafanyakazi saba wa misaada Gaza

2 Aprili 2024

Wafanyakazi saba wa shirika la misaada la World Central Kitchen (WCK) wameuawa hapo jana katika shambulio la anga la Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4eL1m
 World Central Kitchen
Gari la shirika la misaada la World Central Kitchen baada ya kushambuliwa na kombora la Israel na kuwauwa watu saba ndani yake.Picha: Omar Ashtawy/APA Images/ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Shirika hilo limesema wafanyakazi hao walikuwa wakisafiri katika eneo lisilo na migogoro na walitumia magari mawili yenye nembo ya WCK, na licha ya harakati zote kuratibiwa na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF), msafara huo ulishambuliwa ulipokuwa ukitoka kwenye ghala huko Deir al-Balah.

Soma zaidi: Shehena ya kwanza ya misaada kuelekea Gaza yapakuliwa

Mtendaji mkuu wa shirika hilo, Erin Gore, amesema hili si shambulio pekee dhidi ya WCK, bali ni shambulio lisilosameheka dhidi ya mashirika ya kibinaadamu na inadhihirisha hali mbaya inayoendelea na ambapo chakula kinatumiwa kama silaha ya vita.

Mataifa ya Ulaya, China na Australia yamelaani vikali shambulio hilo.

Jeshi la Israel limesema litafanya uchunguzi juu ya mashambulizi hayo, na kuahidi kuchapisha matokeo ya uchunguzi huo kwa uwazi.