JERUSALEM: Olmert kukutana na Abbas | Habari za Ulimwengu | DW | 15.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Olmert kukutana na Abbas

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amekubali kuhudhuria mkutano na rais wa Palestina Mahmoud Abbas utakaoandaliwa na waziri wa masharui ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mkutano kati ya Bi Rice na waziri Olmert mjini Jerusalem hii leo. Haijabainika wazi ni lini na wapi mkutano huo utakapofanyika, lakini maofisa wa Marekani wanaoandamana na Condoleezza Rice katika ziara ya Mashariki ya Kati wamesema mkutano huo utafanyika katika kipindi cha mwezi mmoja.

Akizungumzia kuhusu juhudi za kuutanzua mzozo kati ya Wapalestina na Waisraeli, Condoleezza Rice amesema,

´Bila shaka kwa upande wa usalama ni muhimu sana kuviimarisha vikosi vya usalama vya Palestina. Jenerali Dalton anashirikiana kwa karibu na jeshi la Israel, Misri na vikosi vingine. Kuhusu siasa za ndani ya Israel mimi binafsi zisifuatilii. Hilo ni jambo ambalo waisrael wenyewe wanatakiwa waamue.´

Bi Rice amepangiwa kukutana na rais wa Misri, Hosni Mubarak na katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Amr Moussa baadaye leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com