1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel: Tumemuua kiongozi wa juu wa kijeshi wa Hezbollah

24 Novemba 2025

Jeshi la Israel limesema limemuua kiongozi wa juu wa kijeshi wa Hezbollah katika shambulizi mjini Beirut siku ya Jumapili, ambalo liliwaua watu watano.

https://p.dw.com/p/545WU
Lebanon Beirut 2025 | Wanajeshi wa Hezbollah wakihakikisha usalama eneo lililoko karibu na kuliposhambuliwa na Israel Novemba 23, 2025
Wanajeshi wa Hezbollah wakihakikisha usalama eneo lililoko karibu na kuliposhambuliwa na Israel Novemba 23, 2025Picha: Mohamed Azakir/REUTERS

Haytham Ali Tabatabai, ni kamanda wa juu kabisa wa Hezbollah kuuliwa na Israel tangu walipoanza kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano Novemba 2024, yaliyolenga kumaliza mzozo baina yao uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Taarifa hizo zimethibitishwa pia na kundi hilo la Hezbollah na kuongeza kuwa wapiganaji wake wanne pia waliuawa, huku Wizara ya afya ya Lebanon, ikisema watu wengine 28 walijeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema jana kwamba Israel "haitaruhusu Hezbollah kujiimarisha upya kijeshi", na kutoa wito kwa serikali ya Lebanon "kutimiza ahadi yake ya kuipokonya silaha Hezbollah".