1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aapa kulitokomeza kundi la Hezbollah

23 Novemba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kwamba Israel itafanya kila iwezalo, kuilizuwia kundi la Hezbollah kujiimarisha tena nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/54509
Israel Jerusalem | Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Menahem Kahana/AFP

Netanyahu amesema hatua hiyo itaondoa kitisho cha usalama dhidi ya Israel.

Ndani ya wiki za hivi karibuni Israel imekuwa ikishambulia ngome kadhaa za Hezbollah nchini humo. Hapo jana ilishambulia maeneo ya kijeshi ya kundi hilo la wanamgambo.

Netanyahu ameyasema hayo hii leo alipokuwa anafungua mkutano wa Baraza lake la mawaziri.

Amesema hatua sawa na hizo zitachukuliwa pia dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, alilodai limekuwa likikiuka makubaliano dhaifu ya usitishwaji mapigano yaliyofikiwa kati ya Israel na kundi hilo, na yaliyoanza kutekelezwa Oktoba 10.