1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel: Shambulizi la Iran halitotatiza oparesheni ya Gaza

Amina Mjahid
15 Aprili 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema Israel imefanya mashambulizi ya angani usiku wa kuamkia leo katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4em07
Uharibifu wa mali kwenye Ukanda wa Gaza unaotokana na hujuma za vikosi vya Israel.
Uharibifu wa mali kwenye Ukanda wa Gaza unaotokana na hujuma za vikosi vya Israel. Picha: AFP

Mashambulizi hayo yamefanyika huku jeshi la nchi hiyo likisema halitotatizika katika vita vyake huko, baada ya mashambulizi ya Iran ya siku ya Jumamosi kuongeza hofu ya kutanuka kwa mzozo wa Mashariki ya Kati.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema bado nchi hiyo inaendelea na vita vyake dhidi ya Hamas ikisisitiza kuwa lengo lake ni kuwaokoa watu waliochukuliwa mateka na kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

Huku hayo yakiarifiwa wapatanishi wanaendelea kutafuta makubaliano ya kusitisha vita hivyo huku bado kukiwa na hofu ya Israel kuendelea na mpango wake wa kuishambulia Rafah, kusini mwa Gaza eneo linalowahifadhi wapalestina milioni 2.4 waliokimbia mapigano.