1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yajiandaa kwa uchaguzi unaohodhiwa na wahafidhina

Iddi Ssessanga
28 Februari 2024

Wairan watapiga kura siku ya Ijumaa katika uchaguzi muhimu wa bunge ambapo wahafidhina wanatazamiwa kuimarisha udhibiti wao wa madaraka kutokana na kukosekana kwa ushidani wowote mkubwa.

https://p.dw.com/p/4czoc
Iran Tehran -  Kuelekea uchaguzi wa bunge 2024
Mabango yameonekana kwa uchache safari hii mjini TehranPicha: Yuji Yoshikata/AP/picture alliance

Kiongozi wa Juu wa Jamhuri  hiyo ya Kiislamu Ayatollah Ali Khamenei atakuwa mtu wa kwanza kupiga kura yake majira ya saa mbili asubuhi siku ya Ijumaa, katika moja ya vituo elfu 59 vya kupigia kura.

Katika hotuba mapema mwezi huu, Khamenei alisema kila mmoja anapaswa kushiriki katika uchaguzi huo, akiwahimiza watu wenye ushawishi kuwahimiza watu kupiga kura.

Uchaguzi huo unaofanyika katika hali ya mvutano unaoongezeka kwenye Kanda ya Mashariki ya Kati, unatazamiwa kuhudhuriwa na idadi ndogo ya wapigakura.

Uchunguzi wa maoni ya wapigakura uliofanywa karibuni na kituo cha televisheni a taifa, ulibaini kuwa zaidi ya nusu ya washiriki hawajihusishi na uchaguzi huo.

Iran Teheran | Ali Hosseini Khamenei
Kiongozi wa juu wa Iran Ali Khamenei atakuwa mtu wa kwanza kupiga kura siku ya Ijumaa.Picha: Iranian Leader Press Office/Handout/AA/picture alliance

Zaidi ya watu milioni 61, kati ya wakaazi jumla milioni 85 wa Iran wana vigezo vya kupiga kura.

Bunge la sasa la Iran lililochaguliwa mwaka 2020 wakati janga la Uviko-19, lilishuhudia uitikiaji wa asilimia 42.57, kiwango cha chini kabisaa tangu mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Soma pia: Mhafidhina Ebrahim Raisi ashinda kura ya urais Iran

Mchambuzi wa siasa Ahmad Zeidabadi anasema watu wamekatishwa tamaa  na hali ya kushindwa kwa utawala wa Iran kushughulikia matatizo yao, na kwamba panahitajika maamumuzi ya dhati kwa ngazi ya juu ya kuonyesha wazi azma ya kutaka kutatua matizo, vinginevyo watu wataendelea kujiweka mbali na uchaguzi.

"Katika chaguzi mbili zilizopita idadi ya waliojitokeza kupiga kura imepungua hadi chini ya asilimia 50 na hili linawatia wasiwasi. Huko nyuma mfumo ulihusisha uitikiaji mdogo na janga la Uviko-19 na kutoridhika na serikali iliyopita" alisema Zeidabadi.

Iran Tehran -  kuelekea uchaguzi wa bunge 2024
Hali y akiuchumi ni ngumu kueleka uchaguzi huo wa bungePicha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

"Lakini sasa serikali yao inashikilia madara na ikiwa idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura itapungua, wanahofia shinikizo kutoka mataifa pinzani na wakosoaji wa ndani na itashutumiwa kupoteza msingi wake wa wafuasi. Kwa hivyo wanajali sana, kwa maoni yangu."

Magazeti ya mirengo tofauti yamekuwa na mitizamo tofauti kuhusu uchaguzi huo wa Ijumaa. Gazeti la mrengo wa mageuzi la Ham Mihan liliandika katika chapisho lake la Jumanne kwamba hali ya kisiasa inasalia kuwa ya baridi, likitoa ulinganisho na theluji nzito iliyoanguka nchini Iran katika siku za karibuni.

Soma pia: Ahmadinejad ataka tena urais Iran

Kwa upande mwingine gazeti la kihafidhina la Vatan-e-Emrouz lilisifu kile lilichokiita shauku ya wakaazi katika kampeni za wagombea, zilizoanza Februari 22.

Kutoka wagombea 49,000 hadi 15,000

Katika jiji la Tehran ambako chini ya asilimia 20 ya wapigakura wenye vigezo walipiga kura zad mwaka 2020, mabango ya uchaguzi yanaonekana kwa uchache ikilinganishwa na uchaguzi uliyopita. Wachambuzi watarajia uchaguzi huo kuhodhiwa na wahafidhina na wahadhina wenye misimamo mikali zaidi, sawa na bunge la sasa.

Ayatollah ataka Wahouthi kuungwa mkono

Wagombea walilaazimika kupitia katika mchujo ili kuruhusiwa kugombea nafasi. Majaji waliohusika na mchakato huo wa mchujo waliidhinisha jumla ya wagombea 15,200, idadi hii ikiwa chini ya theluthi moja ya watu 49,000waliojinadikisha kuwania nfasi katika bunge la nchi hiyo lenye jumla ya vita 290.

Soma pia: Rais na bunge waingia kwenye mvutano wa wazi Iran

Wapigakura pia watachagua Baraza la Wataalamu lenye wajumbe 88, ambalo ni chombo muhimu kinachomteua kiongozi wa juu, nafasi inayoshikiliwa tangu mwaka 1989 na Khamenei mwenye umri wa miaka 84.Jumla ya wagombea 144 waliidhinishwa kuwania viti vya baraza hilo kwa muhula wa miaka minane.