1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW yaituhumu Magharibi kwa unafiki juu ya Gaza

20 Oktoba 2023

Human Rights Watch imeituhumu Marekani na mataifa ya Magharibi kwa kile ilichosema ni unafiki na undumilakuwili kwa kushindwa kukemea hatua za kijeshi za Israel katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4XmqL
Gazastreifen | Luftangriff
Mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Naibu Mkurugenzi wa Programu katika shirika hilo la kimataifa, Tom Porteous, amesema tangu Oktoba 7 yalipofanyika mashambulizi ya kundi la Hamas dhidi ya Israel, ni kama kauli za Marekani na Ulaya zimenyamazishwa huku akihoji ni kwa nini vitendo vya kuizingira Gaza kwa miaka 16, ambavyo amesema ni sawa na adhabu ya jumla na uhalifu wa kivita, havikemewi.

Soma zaidi: Ripoti ya Shirika la Amnesty International imeitaja Israel kuwa ni taifa linalozingatia ubaguzi wa rangi

Afisa huyo wa Human Rights Watch amesema kuheshimiwa sheria ya kimataifa juu ya haki za kibinaadamu inayodhamiria kuwalinda raia ni jambo linalowahusu watu wote duniani huku akihoji pia juu ya kukosekana wito ulio wazi kama ilivyokuwa katika mzozo wa Ukraine, wa kuitaka Israel iheshimu kanuni za kimataifa katika mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.