1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hospitali ya Gaza yasema shambulizi la Israel laua watu 20

19 Mei 2024

Hospitali moja ya Ukanda wa Gaza imesema shambulizi la anga la Israeli lililoilenga kambi moja ya wakimbizi katikati mwa eneo hilo la Palestina limewaua watu wasiopungua 20.

https://p.dw.com/p/4g34Q
Ukanda wa Gaza
Mapambano yakiendelea Ukanda wa Gaza Picha: -/AFP

Taarifa ya hospitali hiyo ya Mashahidi wa Al-Aqsa imesema imepokea miili ya watu 20 na wengine kadhaa waliojeruhiwa baada ya ndege za Israel kuilenga nyumba moja kwenye kambi ya wakimbizi ya Al-Nuseirat katikati mwa Gaza.

Mashahidi wamesema shambulizi hilo limetokea mnamo saa tisa za usiku. Jeshi la Israel limesema linachunguza taarifa hizo.

Mapambano makali na mashambulizi mazito ya Israel yamekuwa yakiripotiwa kwenye kambi hiyo tangu Israel ilipoanzisha oparesheni yake ya kijeshi kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah.

Wanamgambo wa Kipalestina wamekuwa pia wakipambana na vikosi vya Israel kwenye kambi nyingine ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.