1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yanaendelea katika mji wa kusini mwa Gaza Rafah

18 Mei 2024

Mapigano makali yameendelea kuutikisa mji wa Rafah Kusini mwa Gaza, wakati serikali ya Israel ikitangaza misaada zaidi kuingizwa katika eneo lililozingirwa kupitia njia iliyotengenezwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4g1gu
Malori ya misaada yaingia mjini Rafah
Malori ya misaada yaingia mjini Rafah Picha: GIUSEPPE CACACE/AFP via Getty Images

Zaidi ya siku 10 ya kile jeshi la Israel ilichosema ni operesheni ndogo ya kijeshi mjini Rafah, mapigano kati ya wanajeshi wa taifa hilo na wanamgambo wa Hamas yameanza tena upande wa Kaskazini mwa Gaza.  

Kulingana na hospitali moja ya kuwait iliyoko katika eneo hilo, mashambulizi ya usiku kucha yamesababisha mauaji ya watu wawili katika kambi inayowahifadhi watu waliokosa makaazi mjini Rafah.

WHO yaonesha hofu juu ya ukosefu wa misaada Gaza

Makundi ya kutoa misaada yamesema operesheni ya Israel mjini Rafah inafanyika licha ya miito chungu nzima ya kimataifa ya kuipinga na huku wapatanishi wakijaribu kuyafufua mazungumzo yaliyokwama ya kusitisha mapigano.

Wamesema kile kinachoonekana sasa huenda kikafanya hali ya kibinaadamu kuwa mbaya zaidi katika ukanda wa Gaza.