1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Hofu yatanda juu ya kushambuliwa kinu cha Zaporizhzhia

Sudi Mnette
5 Julai 2023

Urusi na Ukraine zimetupiana lawama kuhusu njama za kufanya mashambulizi katika eneo la kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kinachodhibitiwa na Urusi baada ya uvamizi wake.

https://p.dw.com/p/4TRTK
Ukraine Kernkraftwerk Saporischschja
Picha: Dmytro Smolyenko/Ukrinform/abaca/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amemwambia mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, juu ya vitendo vya kichokozi vya Urusi katika maeneo ya kinu hicho huko kusini mashariki mwa Ukraine. Kupitia ukurasa wake wa Tweeter, Zelenskiy ameandika kuwa alimwambia Macron kwa njia ya simu kwamba askari wakaliaji wa Kirusi wanaandaa shambulizi la hatari katika eneo la Zaporizhzhia.

Ikimbukwe tu kwamba Urusi ilifanikiwa kukiteka kiwanda hicho kikubwa kabisa cha nyuklia barani Ulaya, chenye vinu sita, baada ya uvamizi wa Februari 2022. Mara kwa mara kwa kila upande umekuwa ukishutumu mwingine kwa kuvurumisha makombora kwenye maeneo ya karibu na kiwanda hicho na kuhatarisha ajali kubwa ya nyuklia.

Zelensky: Tuna taarifa za kijasusi.

Ukraine Wolodymyr Selenskyj
Raisa wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrinform/ABACA/IMAGO

Kuhusu lawama hizo za hivi punde kwa upande wa Ukraine Rais Zelensky anasema "Tuna taarifa kutoka katika kitengo chetu cha ujasusi kwamba vikosi vya Urusi vimeweka vitu vinavyofanana na viripuzi kwenye mapaa ya maeneo kadhaa ya kinu cha nyuklia wa Zaporizhzhia. Inaweza kuwa ni kufanikisha shambulizi katika eneo hilo. Lakini kwa hali yoyote, ulimwengu unashuhudia. Chanzo pekee cha hatari katika kinu cha Zaporizhzhia ni Urusi na hakuna kingine chochote

Nae Renat Karchaa ambae ni mshauri wa mkuu wa Rosenergoatom, ofisi ambayo inaendesha mtandao wa nyuklia wa Urusi, anasema Ukraine imepanga kufanya njama za mashambulizi kwa kuingiza silaha husika kutoka katika taifa lingine. Anasema  kwa kificho, usiku wa leo hii jeshi la Ukraine litafanya jaribio la kulishambulia eneo la Zaporizhzhia kwa kutumia makombora ya masafa marefu.

Hisia za Urusi kwa sambulizi la Zaporizhzhia.

Hata hivyo Karchaa ambae alionekana akiyasema hayo katika televisheni ya Urusi hakuwa na ushahidi wowote ya kuthibitisha kauli yake. Kwa zaidi ya mwaka mmoja shirika la uangalizi wa nguivu za atomiki la Umoja wa Mataifa,IAEA, limekuwa likijaribu kuzua eneo hilo kutokwa la nguvu za kijeshi ili kupunguza hatari za ajali yoyote ya nyuklia.

Soma zaidi:Katibu mkuu wa NATO kubakia madarakani kwa mwaka mwingine

Katika hatua nyingine Urusi imeonesha ishara ya kutoendelea na utekelezaji wa makubaliano ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka ya Ukraine kupitia Bahari Nyeusi, ambayo tamati yake kwa sasa itakuwa Julai 17. Pamoja na madai yaliopo na mengine mapya, uongozi wa Urusi unautaka Umoja wa Mataifa kufanya jitihada zaidi kuondoa vikwazo katika mauzo ya bidhaa zake kwa nje ya taifa hilo.

Vyanzo: RTR/DPA