1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Hezbollah yavurumisha maroketi 100 katika milima ya Golan

Josephat Charo
12 Machi 2024

Kundi la Hezbollah linaloegemea Iran limefyetua maroketi kiasi 100 aina ya Katyusha kwenye kambi mbili za jeshi la Isreal katika milima ya Golan hivi leo.

https://p.dw.com/p/4dRHf
Hezbollah yavurumisha maroketi 100 katika milima ya Golan
Hezbollah yavurumisha maroketi 100 katika milima ya GolanPicha: Taher Abu Hamdan/Xinhua/picture alliance

Hezbollah imesema hatua hiyo ni ya kulipiza kisasi shambulizi la kutokea angani lililofanywa na Israel ambalo lilimuua raia mmoja katika mji wa Baalbeck, mashariki mwa Lebanon Jumatatu jioni. Kwa mujibu wa duru za usalama za Lebanon watu wengine sita walijeruhiwa katika shambulizi hilo. Hakukuwa na ripoti zozote za majeruhi wala uharibifu upande wa Israel.

Israel imesema imeishambulia mitambo mitatu ya kuvurumishia maroketi nchini Lebanon iliyokuwa inatumiwa kufyetua maroketi kuelekea milima ya Golan leo asubuhi.