MigogoroLebanon
Hezbollah yaionya serikali inayolenga kudhibiti silaha zaidi
14 Januari 2026
Matangazo
Taarifa hii ni kulingana na maoni yaliyosambazwa na kundi hilo lenye silaha leo Jumatano.
Kundi hilo limeahidi kuziweka silaha zote chini ya udhibiti wa serikali, kufuatia makubaliano ya 2024 yaliyomaliza vita vikali kati ya Hezbollah na Israel
Katika mahojiano na chombo cha habari cha serikali ya Urusi RT, afisa mwandamizi wa kisiasa wa Hezbollah Mahmoud Qmati alisema ikiwa watataka pia kudhibiti silaha kwenye eneo la kaskazini itakuwa ni "uhalifu mkubwa zaidi" unaofanywa na serikali.
Hezbollah inasisitiza kwamba makubaliano hayo yanapaswa kutumika tu kwenye eneo la kusini mwa Lebanon linalopakana na Israel na limekataa kusalimisha silaha zake kwenye maeneo mengine.