1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G20 yasema ni muhimu kudhibiti covid ili kusaidia uchumi

Iddi Ssessanga
14 Oktoba 2020

Wakuu wa sekta ya fedha kutoka mataifa ya kundi la G20 wamesisitza haja ya kudhibiti kuenea kwa janga la virusi vya corona, na wameahidi kufnya kila liwezekanalo kusaidia uchumi wa dunia na utulivu wa sekta ya fedha.

https://p.dw.com/p/3jw1E
Saudi Arabien | G20-Finanzministertreffen in Riad
Picha: Getty Images/AFP/F. Nureldine

Katika taarifa ndefu, mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za mataifa ya G20 wamesema wataendelea kushughulikia athari zisizolingana na mzozo wa janga la covid-19 kwa wanawake, watu wenye umri mdogo na makundi mengi ya kijamii yalioko hatarini duniani.

Wamekubaliana pia kurefusha mpango wa usitishaji malipo ya mikopo katika mataifa kwa muda wa miezi sita, kutokana na shinikizo la kifedha linaloyakabilia mataifa yenye kipato kidogo, na wameelezea kuvunjwa moyo na kutokuwepo kwa wakopeshaji wa sekta binafsi katika mpango huo.

Soma pia: Watu mashuhuri 225 wataka mataifa tajiri kusaidia masikini

Mazungumzo hayo ya mtandaoni, yaliyoitishwa na rais wa kundi hilo Saudi Arabia, yamekuja siku moja baada ya shirika la fedha la kimataifa IMF, kuonya kwamba pato jumla la ndani la dunia litanywea kwa asilimia 4.4 mwaka huu wa 2020, na athari za hasara iliyosababishwa na janga la covid-19 zitaendelea kwa miaka kadhaa.

Saudi Arabien | G20-Finanzministertreffen in Riad
Saudi Arabia ndiyo rais wa kundi la G20 kwa sasa.Picha: Imago iIages/photothek/F. Gärtner

Waandaji wa mkutano huo wa G20 walisema katika taarifa kwamba mkutano huo unajadili taarifa mpya za mpango kazi wa G20 -- ambazo ni kusaidia uchumi wa dunia kupita katika janga la covid-19.

Soma pia: Kundi la G20 kusaidia soko la ajira lisiporomoke

Mataifa 20 yaliostawi zaidi kiviwanda duniani na yanayoinukia kiuchumi yaliahidi mwezi Aprili kusitisha ulipaji madeni kwa mataifa maskini zaidi hadi mwishoni mwa mwaka huu kwa sababu ya kunywea vibaya kwa uchumi kulikosababishwa na janga la covid-19.

Wapiga kampeni wataka ulipaji madeni usitishwe hadi 2020

Benki ya dunia na makundi ya kampeni wametoa wito wa kurefushwa kwa mpango huo wa usitishaji wa malipo ya madeni hadi mwishoni mwa mwaka 2021, huku mashirika ya hisani kama vile Ofam yakisema unahitaji kurefusha hadi 2022.

Screenshot Website G20 Interfaith Forum, Riyadh, Saudi-Arabien
Mkutano wa mawaziri wa fehda na wagavana wa benki kutoka mataifa ya G20 wamehudhuria mkutano ulioongozwa na Saudi Arabia.Picha: g20interfaith.org

Lakini rais wa benki ya dunia David Malpass siku ya Jumatatu alionya kuwa nchi za G20 zinaweza kuidhinisha urefushaji wa miezi sita tu kwa sababu siyo wakopeshaji wote wanashiriki kikamilifu kusaidia mataifa maskini kukabiliana na mzozo huo wa kiafya.

Soma pia: IMF na kundi la G-20 zatoa nafuu kwa mataifa masikini

G20 ilisema mwezi Septemba kwamba mpango wa DSSI ulipokea maombi 46 kutoka mataifa yenye vigezo kote duniani, mengi kutoka barani Afrika. Lakini wapiga kampeni wa kimataifa wamelikosoa kundi hilo kwa kutofanya vya kutosha kuyasaidia mataifa maskini kushughulikia athari za janga la covid-19.

Soma pia:Viongozi wa ulimwengu waapa kupambana na COVID-19

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na waziri wa fedha wa Saudi ArabiaMohammed-al-Jadaan na gavaba wa benki kuu Ahmed al-Kholifey, yamekuja wakati ambapo mzozo wa kiafya  wa covid-19 ukiendelea kuuathiri uchumi wa dunia, na kusababisha ukosefu wa ajira wa viwango vya kihistoria.

Chanzo: Mashirika