Frayser-Price bingwa wa dunia kwa mara ya nne
30 Septemba 2019Matangazo
Frayser-Price mwenye miaka 32 ambaye hakushiriki mashindano ya mwaka 2017 kwasababu alikuwa mja mzito, alitimka kwa muda wa sekunde 10.71 na kunyakua dhahabu.
Dina Asher-Smith wa Uingereza akaichukua nafasi ya pili na nishani ya shaba ikachukuliwa na Muivory Coast Marie-Josee Ta Lou.
Rekodi ya Usain Bolt ya medali za dhahabu ilivunjwa Jumapili pia na mwanadada wa Marekani Allyson Felix ambaye pia alikuwa anarudi kutoka kwenye likizo ya uzazi.
Timu ya Marekani aliyokuwemo Felix ilishinda dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti za mchanganyiko wa wanawake na wanaume kwa wakimbiaji wanne kwa mita mia nne.