FIFA yapinga kauli ya Maradona | Michezo | DW | 05.07.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

kombe la dunia 2018

FIFA yapinga kauli ya Maradona

Shirikisho la Soka Duniani FIFA limesema linazipinga kwa nguvu zote kauli za nyota wa zamani wa soka wa Argentina, Diego Maradona, kwamba ushindi wa timu ya Uingereza dhidi ya Colombia ni wizi.

Aidha, Maradona alidai kwamba refa Mark Geiger hakuwa na viwango vya kusimamia mchezo huo. FIFA imesema kauli ya Maradona haikubaliki na haina msingi wowote. Uingereza ilishinda mechi hiyo kwa mikwaju ya penalti baada ya kumalizika dakika 120 za mchezo. FIFA pia imesema inafanya kila iwezalo kuhakikisha sheria ya Fair Play, uadilifu na heshima vinazingatiwa katika michuano ya Kombe la Dunia 2018.