1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yamtishia vikwazo vipya Lukashenko

9 Agosti 2021

Mwaka mmoja tangu alipochaguliwa tena, rais wa Belarus Alexander Lukashenko ametishiwa kukabiliwa na vikwazo vipya kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya

https://p.dw.com/p/3ylX2
Weißrussland | Präsident Alexander Lukaschenko
Picha: Pavel Orlovsky/AP Photo/picture alliance

Mamia ya Wabelarus wanaoishi uhamishoni nchini Poland wakiandamana kupinga ukandamizaji wa kisiasa. Soma Mwanaharakati wa Belarus apatikana amekufa Ukraine

Mkuu wa Sera za kigeni wa Umoja Ulaya Josep Borell amesema umoja huo uko tayari kuzingatia hatua zaidi kwa utawala wa Belarus kwa kudharau wazi wazi kanuni za masharti ya kimataifa.

Borell ameongeza kuwa pamoja na kulazimishwa kinyume cha sheria kutua kwa ndege ya Ryanair mnamo Mei na kutumia wahamiaji kwa madhumuni ya kisiasa, serikali ya Belarus imekuwa ikikiuka kanuni za kimataifa.

Borrell amegusia kati ya mambo mengine, kwamba visa vya wahamiaji haramu zaidi ya 2,000 vilisajiliwa kwenye mpaka wa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya Lithuania na Belarusi mwezi Julai peke yake.

Kusudi ya serikali ya Belarus

Berlin I Kundgebung der weißrussischen Opposition
Picha: Vladimir Esipov/DW

Kwa mujibu wa Umoja wa Ulaya Serikali ya Minsk inafanya makusudi na Lukashenko alikuwa ametishia kwamba ataruhusu watu kutoka nchi kama Iraq, Afghanistan au Syria kuvuka mpaka ili kujibu vikwazo.

Mnamo Agosti mwaka 2019, Lukashenko alitangazwa mshindi kwa asilimia 80.1 ya kura licha ya shutuma kubwa za ulaghai wakati wa uchaguzi, huku maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yakizimwa kwa ukatili.

Umoja wa Ulaya haumtambui tena Lukashenko kama rais na tayari vikwazo vimewekwa katika miezi ya hivi karibuni juu ya ukandamizaji wa raia na kuminywa demokrasia nchini Belarusi. Hivi karibuni pia kumekuwa na vikwazo vya kiuchumikufuatia kukamatwa kwa mwanahabari anayepinga serikali Roman Protasevich.

Mwanariadha akimbilia uhamishoni

Polen/Belarus Die Sportlerin Kristina Timanowskaja und belarussische Oppositionspolitiker Pawel Latuschko bei der Pressekonferenz
Kristina TimanowskajaPicha: Magdalena Gwozdz/DW

Kisa cha hivi karubuni cha mwanariadha wa Olimpiki wa Belarus Kristina Timanovskaya pia kilionyesha kuwa mtu yeyote anaweza kuwa mwathirika wa ukandamizaji wa Lukashenko.

Huku hayo yakijiri waandamanaji walikusanyika katikati mwa mji wa Warsaw nchini Poland, wakipita karibu na ubalozi wa Marekani na Urusi wakilenga ubalozi wa Belarus katika wilaya ya kusini mwa Warsaw. soma Viongozi walaani kukamatwa mwanaharakati wa Belarus

"Hatuwezi kukubali na kujifanya kuwa hakuna kinachotokea, tunapaswa kupigana. Sasa jukumu linatuangukia tulio nje ya nchi kwa sababu huko Belarus watu hawawezi kuandamana kwasababu watatupwa gerezani," alisema Frantz Aslauki, mjasiriamali kutoka mji wa Wroclaw ambaye alikuwa miongoni mwa waandamanaji.

"Tunayo nafasi ya kuonyesha kwa hivyo jukumu hili liko juu yetu, lazima tupaze sauti kwa ulimwengu wote, ili ulimwengu wote utuunge mkono katika kutafuta uhuru na demokrasia, " aliogeza kusema mwandamanaji huyo raia wa Belarus.

Waziri wa mambo ya nje wa UjerumaniHeiko Maas ameahidi kuunga mkono harakati za demokrasia akisema kuwa Lukashenko ameiweka Belarus mateka.

 

Vyanzo/DPA,AP