1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droni za Urusi zauwa 4, zajeruhi 12 Kharkiv

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Watu wanne wameuwawa na wengine 12 wamejeruhiwa katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine kufuatia shambulizi la droni lililofanywa na Urusi.

https://p.dw.com/p/4ePy6
Ukraine Kharkiv
Jengo lililoshambuliwa na droni za Urusi mjini Kharkiv, mashariki mwa Ukraine siku ya Alkhamis (4 Aprili 2024).Picha: Sergey Bobok/AFP

Gavana Oleh Syniehubov na Meya Ihor Terekhov walitangaza kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram asubuhi ya Alkhamis (Aprili 4) kwamba raia mmoja na maafisa watatu wa uokoaji ni miongoni mwa waliouliwa katika eneo hilo lenye makaazi ya raia.

Kwa mujibu wa maafisa, majengo kadhaa yaliharibiwa likiwemo jengo la ghorofa nyingi lenye makaazi ya watu.

Soma zaidi: Urusi yaionya Ufaransa fikra ya kupeleka wanajeshi Ukraine

Kati ya droni 20 ambazo Urusi ilizitumia kuishambulia Ukraine usiku wa kuamkia Alkhamis, 15 zilielekezwa katika mji wa Kharkiv.

Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine ulifanikiwa kuzidunguwa baadhi ya droni hizo.