1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine

3 Oktoba 2025

Urusi imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine katika maneo kadhaa usiku wa kuamkia Ijumaa 03.10.2025. Hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya miundombinu ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/51SRt
Kharkiv, Ukraine 2025
Juhudi za kuzima moto zikiendelea baada ya moja ya mashambulizi ya Urusi nchini UkrainePicha: Sergey Bobok/AFP

Kulingana na mamlaka nchini humo, Urusi ilifanya mashambulizi kwa kutumia droni 381 na makombora 35 yaliyoilenga miundombinu hiyo kwenye mikoa ya Kharkiv na Poltava iliko mitambo mikubwa ya kuzalisha gesi.

Shughuli za kampuni ya mafuta na gesi za DTEK zasitishwa

Kufuatia mashambulizi hayo, Kampuni kubwa zaidi binafsi ya mafuta na gesi ya Ukraine DTEK imetangaza kupitia jukwaa la X kuwa sitisha shughuli zake katika baadhi ya vituo vyake katika mkoa wa Poltava baada ya mashambulizi ya Urusi.