1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Demokrasia inakabiliwa na kitisho kote ulimwenguni

Grace Kabogo
19 Machi 2024

Kwa miongo miwili Wakfu wa Bertelsmann wa nchini Ujerumani Ujerumani umekuwa ukiyafuatilia mataifa 140 kwa lengo la kubaini iwapo yanaelekea kwenye utawala wa kidemokrasia au yanaongoza kimabavu.

https://p.dw.com/p/4dtoH
Kenya-Uchaguzi mkuu 2022
Uchaguzi wa Kenya 2022Picha: IMAGO/ZUMA Wire

Utafiti mpya uliofanywa hivi karibuni na Wakfu wa Bertelsmann umeonyesha matokeo ya kutia wasiwasi na umefichua kuwa ubora wa demokrasia umeshuka katika kipindi cha miaka 20 iliyopita kwenye nchi 137 ambazo zinachukuliwa kama zinazoendelea au zinazoinukia kiuchumi.

Kulingana na "Faharasa ya Mabadiliko" ya Wakfu wa Bertelsmann, kwa sasa kuna nchi 63 zinatofuata demokrasia ikilinganishwa na nchi 74 zinazoongozwa kwa mkono wa chuma. Kwa maneno mengine, ni mataifa ambayo hayafanyi uchaguzi huru au hayana serikali zinazofuata katiba.

Soma: Viongozi waungane kumaliza changamoto za demokrasia na usalama, Afrika.

Kulingana na utafiti huo, katika miaka miwili iliyopita pekee, iliyochangiwa na hali mpya ya kisiasa na kijiografia, uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na janga la virusi vya corona, uchaguzi katika nchi 25 umekuwa usio huru na wa haki, kuliko ilivyokuwa awali. Aidha, uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo  vya habari kwenye nchi 39 umekuwa ukidhibitiwa zaidi.

Afrika Kusini-Chanjo ya corona
Watu waliopatiwa chanjo ya corona Afrika KusiniPicha: Jerome Delay/AP Photo/picture alliance

Sabine Donner ni mmoja wa waliofanya utafiti huo. Ameiambia DW kuwa janga la virusi vya corona limeathiri maendeleo ya kidemokrasia kutokana na kufungwa kwa shughuli za umma na kuwekwa kwa muda vizuizi vya watu kutembea.

Tanzania: Tanzania yaadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani ikielekea kwenye uchaguzi

''Janga la corona lilikuwa fursa ya kuzuia zaidi haki na kuelekeza nguvu zaidi mikononi mwa serikali. Lakini kimsingi, janga hilo halikuleta matatizo yoyote ambayo hayakuwepo kabla," alifafanua Sabine.

Ripoti ya 2022: Ripoti: Nusu ya mataifa ya kidemokrasia duniani yanashuka

Kwa mujibu wa Wakfu wa Bertelsmann, utafiti wao wa kila mwaka ndiyo mkubwa zaidi na wa kina. Ripoti ya utafiti huo yenye kurasa 5,000, umefanywa kwa msaada wa wataalamu 300, vyuo vikuu na taasisi kwenye takribani nchi 120. Utafiti unaangazia mabadiliko ya kisiasa kuelekea demokrasia, mabadiliko ya kiuchumi, na hatua za kiserikali.

Ukraine I wakimbizi
Wakimbizi wa Ukraine Picha: Dominika Zarzycka/ZUMA/IMAGO

Sabine anasema katika kipindi cha miaka miwili hadi minne iliyopita, watu na serikali zimefahamu zaidi changamoto za utawala wa kimabavu ambazo zinazikabili nchi za kidemokrasia ikiwemo Ujerumani. Anasema wana ufahamu zaidi sasa kuliko walivyokuwa miaka 10 iliyopita.Utafiti: Viwango vya demokrasia vimeshuka ulimwenguni katikati mwa vita

Wakfu wa Bertelsmann ulimualika Kansela wa Shirikisho la Ujerumani, Olaf Scholz wa chama cha Social Democratic, SPD, wakati ukiwasilisha utafiti wao siku ya Jumatatu. Kutokana na kuongezeka kwa siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani, Scholz amesema amefurahishwa na hatua ya maelfu ya watu hivi karibuni kujitokeza mitaani kupinga hilo.

Watawala wa kimabavu huwa wanapenda kuhalalisha vitendo vyao wakidai kuwa michakato ya kidemokrasia ni migumu sana, kwamba serikali zilizochaguliwa kidemokrasia hazibadiliki, na nchi zao haziwezi kuendana na kasi ya ushindani wa kimataifa. Kwa mujibu wa Sabine, namna China ilivyolishughulikia janga la UVIKO-19 imeonyesha kuwa tawala za kimabavu hazitumii busara ikilinganishwa na zile zinazofuata demokrasia wakati wa mizozo.

Düsseldorf -maandamano- Corona
Maandamano ya kupinga chanjo ya corona UjerumaniPicha: Roberto Pfeil/dpa/picture alliance

Suala la msingi la kupambana na utawala wa kiimla linabakia kuwa dhamira ya kiraia kwa kufanyika uchaguzi huru, uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na mgawanyo wa madaraka. Iwapo kuna uungaji mkono wa umma kwenye maeneo hayo, huenda ikasaidia kuzuia utawala wenye mwelekeo wa kimabavu.ICC yasitisha uchunguzi machafuko baada ya uchaguzi Kenya.

Mo Ibrahim: Mapinduzi ya kijeshi yameshamiri AfrikaUtafiti huo umezitolea mfano uchaguzi wa hivi karibuni nchini Kenya na Zambia, pamoja na Poland na Moldova barani Ulaya. Sabine anazitolea mfano nchi ambazo zilibadilika kwa mafanikio hadi kwenye mifumo ya kidemokrasia ikiwemo Taiwan au Korea Kusini, ambazo zilikuwa chini ya utawala wa kiimla kwa muda mrefu na sasa zina demokrasia thabiti na zenye mafanikio.

Faharasa ya Mabadiliko ya mwaka 2024 zinazielezea Korea Kusini, Costa Rica, Chile, Uruguay, na Taiwan kama nchi zilizozingatia utawala wa sheria na kwa mtazamo wa kimkakati, na uongozi wao wa serikali umehakikisha kufikiwa kwa maendeleo mazuri sio tu katika elimu, huduma za afya, na viwango vya maisha, lakini pia katika kuimarisha demokrasia."