1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaraka ya kimabavu Afrika yanasababisha itikadi kali

Sudi Mnette
10 Julai 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema vurugu za serikali na matumizi mabaya ya madaraka barani Afrika vinaweza kutoa msukumo wa jamii kuingia katika mambo ya kuwasukuma itikadi kali. 

https://p.dw.com/p/3LryF
International Charlemagne Prize Of Aachen 2019
Picha: Getty Images/. Ebener

hayio ameyasema katika mkutano wa kupambana na ugaidi uliofanyika Nairobi Kenya. Amesema ukosefu wa elimu na umaskini ni miongoni mwa mambo ambayo yanawýeowza kuwaingiza watu wa bara la Afrika kwenye dimbwi la itikadi kali, na kuongeza kuwa pamoja na hilo chanzo kikubwa kwa sehemu kubwa ni  ukandamizaji wa serikali pamoja na matumizi yake mabaya ya madaraka.

Majeshi ya mataifa matano ya Afrika Magharibi yanazidiwa nguvu

Kenia Garissa Polizei Soldat
Mwanajeshi wa Kenya katika eneo la GarissaPicha: picture-alliance/dpa/D. Irungu

Guterres amesema hakuna kinachoweza kuhalalishaugaidi na itikadi za vurugu, lakini akasisitiza ukweli kwamba hayo hayatokei hivihivi tu. Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amezungumzia kuenea kwa ugaidi barani Afrika, hasa katika kanda ya Sahel. Pia amelitaja kundi la Boko Haram nchini Nigeria, na mashambulizi ya hivi karibuni nchini Kenya, Mali, Niger na Burkina Faso. Kutoka na hali hiyo ameitaka jumuiya ya kimataifa kuyaunga mkono mataifa hayo ya Afrika Mashariki ili kukabiliana na vurugu zitokanazo na itikadi kali.

Aidha amesema pamoja na jitihada zilizopo sasa katika eneo hilo lakini nguvu ya makundi ya wenye itikadi kali inazidi kuongezeka na kupata nguvu katika eneo kubwa la Sahel, jambo ambalo linasababisha idadi kubwa ya watu kuyakimbia makazi yao. Kwa hivi sasa jeshi la pamoja la Mali, Burkina Faso, Nigeri, Chad na Mauritania lenye lengo la kukabiliana na makundi ya wapiganaji linahitaji nguvu ya ziada kutoka nje.

Akizungumza katika mkutano huo wa kukabiliana na ugaidi Guterres amesema "Walianzia Mali, wakielekea Burkina Faso, Niger na sasa tukizungumza na rais wa Ghana, Benin, Togo na Ivory Coast wanasema ugaidi unakaribia katika mipaka yao" alisema Guterres.

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliongeza kwa kusema ni muhimu kwa majeshi ya Afrika kuwa na mamlaka stahiki na fedha za kutosha, kufanya kazi yao, na kutoa wito wa jitihada za pamoja na kukabiliana na makundi ya itikadi kali nje ya jeshi la pamoja linaloundwa na matiafa ya G-5. Mkutano huo wa siku mbili unawajumuisha wadau mbalimbali kutoka pande tofauti za ulimwengu.

Vyanzo: DPA/AFPE