China na Tibet | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

China na Tibet

Je, michezo ijayo ya olimpik nchini china isusiwe au siasa mbali na michezo mbali ?

default

Watibeti waandamana

Picha zinazoonesha magari yaliopinduliwa na kubomolewa,maduka yanayowaka moto,ripoti za kufyatuliwa risasi waandamanaji na mkomoto pamoja na idadi inayotatanisha ya watu wangapi wameuwawa ni vichwa vya habari kutoka Tibet-mkoa unaolilia uhuru wake kutoka China.Kile ambacho kilianza kwa maandamano ya amani kupinga utawala wa China huko Tibet kiligeuka kihoro cha matumizi makubwa ya nguvu kutoka pande zote mbili.

Kwa mara nyengine tena Tibet imejitokeza mbele ya macho ya walimwengu na kile ambacho China ikijaribu kukizuwia -kuchanganya michezo ijayo ya olimpik na madai ya kuheshimu haki za binadamu na siasa kimeibuka tena:

Uchambuzi wa Matthias von Hein mnasimuliwa studioni na

Kila kitu sio tu kingeenda vyema na kuwa bambamu,bali kilibidi kwa kila hali, kiende vyema,kwani Machina wamekamia iwe hivyo. Matumizi makubwa ya kuandaa michezo ijayo ya olimpik mjini Beijing,

yalipindukia na imani mpya iliojipatia China ulimwenguni.

China ilikamia kuutembeza mji wake mkuu -Beijing kuwa mji wa kisasa kabisa hirimu saswa na miji mikubwa duniani na mwishoe imezikaribia dola kuu baada ya juhudi za miongo 3 tu za kustawisha uchumi wake.

Lakini sasa mabo yameichachia,kwani hakuna anaonesha hamu ya viwanja vyake vya kimamboleo vya michezo na pazia lake la makaribisho ya kuonesha kuwa nchini china wananchi wake wa jamii mbali mbali wanaishi kwa pamoja na kwa amani.

Waandamanaji wametoa picha tofauti kabisa za sura ya china -nayo kuwa China inakandamiza upinzani wowote ule unaoibuka na hata ukiwa unaoneshw akwa njia za amani.walimwengu wamestushwa kujionea picha za watibeti waliozusha machafuko na kuchoma moto maduka.Kuzidi machafuko ya nguvu ni matokeo ya kuwaandamana kupita kiasi kwa wale wenye maoni tofauti na ya watawala.

Mkomoto unaoendeshwa na vikosi vya usalama dhidi ya wakunga wa dini ya budha walioandamana kuliongoza kwa chungu kilichokua kikitokota sasa kumwsaika.Kwani ghadhabu zilizomezwa muda mrefu sasa zimeripuka mjini Lahsa kuwapinga wahamiaji kutoka sehemu nyengine ya China katika sehemu yao ya Tibet.

Uongozi wa Beijing hauchoki kupiga upatu mafanikio gani ya kiuchumi Tibet imejipatia kama sehemu ya China.Tarakimu za ufanisi kwa kweli zinavutia.Lakini kustawi huko kwa uchumi na neema yake hawaioni wazalendo wa Tibet.Wenyeji wa Tibet huwa ni vibarua tu au watemebzi wanaowaongoza watalii peponi.

Hakuna shaka serikali ya China imefanya juhudi kubwa kuboresha hali za maisha huko Tibet ,hali ambazo chini ya utawala wa Lama hazikuwa bora kinyume na vile unavyosikia katika nchi za magharibi.

Ni kwa jicho hilo China haielewi kwanini watibeti hawsawashukuru.

Ukweli wa mambo si taabu kuona:Watibet hawakuwaalika machina kwao wawatawale.Hawakuulizwa ndewe wala sikio.Mtu mwenye madaraka makubwa huko Tibet ni Katibu mkuu wa chama na wakati wote ni mchina sio mtibeti.Hata Hu Jintao aliechaguliwa mwishoni mwa wiki rais wa china kwa kipindi cha miaka 5 mengine aliwahi mkushika wadhifa huo wa katibu mkuu wa chama.

1989 ndie alieamrisha kukandamizwa kwa mabavu maandamano ya watibeti .

kutumia tena mkono wa chuma bila ya kujali walimwengu na kukandamiza vilio vya watibeti mara hii kama wakati ule haimudu tena China.kwani, leo kila kichochoro na kila pembe kuna kamera za simu ya mkonona leo kuna wasafiri wengi huko-mashahidi wa yanayotokea.Hatahivyo, Chjina haitaacha kutumia mkomoto kuzima sauti za watibeti.

Kususia michezo ijayo ya olimpik ya Beijing si sawa na hii anaungama hata kiongozi wao watibeti Dalai lama.Juhudi zote ilizofanya China hazikufaulu kuzima jaribio la kuchanganya michezo na siasa-olimpik na haki za binadamu.Silaha hiyo katika kutetea haki za binadamu nchni China ni halali kuitumia.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com