SiasaChile
Chile yaunga mkono kesi dhidi ya Israel huko ICJ
2 Juni 2024Matangazo
Akihutubia bunge la nchi yake Jumamosi (01.06.2024), Boric alishutumu hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza na kutoa wito wa majibu madhubuti kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.
Rais wa Chile amesema nchi yake itakuwa mshiriki na kuunga mkono kesi ambayo Afrika Kusini iliwasilisha dhidi ya Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague.
Mahakama ya ICJ inazingatia kesi ya Afrika Kusini, lakini kwa muda mfupi imetoa uamuzi wa awali kuiamuru Israeli kufanya kila iwezalo kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki wakati wa operesheni yake dhidi ya Hamas.
Nchi ya Chile imeitambua Palestina kama taifa tangu mwaka 2011, na rais Gabriel Boric alishawahi kusema kuwa vita vya Gaza "havina uhalali" na "havikubaliki."