1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Chama tawala Urusi chakumbwa na shambulio la mtandaoni

16 Machi 2024

Chama tawala cha Urusi kimesema leo kuwa kimekumbwa na shambulio kubwa la mtandaoni ambalo limelemaza huduma za Intaneti.

https://p.dw.com/p/4dngy
Wafanyikazi wa tume ya uchaguzi ya Urusi
Wafanyikazi wa tume ya uchaguzi ya UrusiPicha: Alexandr Piragis/Sputnik/IMAGO

Chama hicho tawala kimesitisha utoaji wa huduma zisizokuwa za msingi ili kudhibiti shambulio hilo.

Rais Vladimir Putin ambaye anatetea kiti chake kama mgombea huru japo anaungwa mkono na chama tawala cha United Russia, ameishtumu Ukraine kwa kujaribu kuhujumu uchaguzi huo ambao anatarajiwa kushinda.

Soma pia: Ni yapi malengo ya Rais Putin kwa kuandaa uchaguzi nchini Urusi? 

Uchaguzi huo wa siku tatu ulioanza jana, pia unafanyika katika maeneo manne ya Ukraine - Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson.

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini Urusi, takriban watu milioni 112 wamejiandikisha kama wapiga kura.