CCM yakiri kupoteza Arumeru Mashariki kwa CHADEMA | Matukio ya Afrika | DW | 03.04.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

CCM yakiri kupoteza Arumeru Mashariki kwa CHADEMA

Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilimtangaza Joshua Nasari, mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana Jumapili, akimshinda Sioi Sumari wa CCM.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

CCM imekubali kupoteza jimbo hilo, huku msemaji wake, Nape Nnauye, akisema kwamba bado si dalili ya kupoteza nguvu kwa chama chake. Mwandishi wetu aliye jimboni Arumeru, Dotto Bulendu, anasema hali leo ni shwari baada ya hapo jana kuwepo kwa vurugu kidogo.

Mgombea wa CHADEMA amepata asilimia 54 na CCM kupata asilimia 44. Chama cha CCM kiko madarakani tangu kilipoasisiwa mwaka 1977 kikiwa kimerithi kutoka waasisi wake, vyama vilivyopigania uhuru katika pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, TANU kwa iliokuwa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Dotto Bulendu
Mhariri: Saumu Yusuf

Sauti na Vidio Kuhusu Mada