Carter awasili Jordan kuzungumza na Mfalme Abdullah II | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Carter awasili Jordan kuzungumza na Mfalme Abdullah II

Amman:

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amewasili mji mkuu wa Jordan-Amman,sehemu ya ziara yake ya kutathimini hali ya mambo katika Mashariki ya kati. Bw carter akitarajiwa kuwa na mazungumzo na Mfalme Abdullah II na wanasiasa wa ngazi ya juu wa Jordan, kuwaarifu juu ya mazungumzo yake na Kiongozi mkuu wa chama cha Hamas Khalid Mashaal katika mji mkuu wa Syria-Damascus pamoja na pendekezo lake la usimamisha mapigano katika ukanda wa Gaza.

Hadi sasa Bw Carter ameshazizuru Israel, Misri, Syria na Saudi arabia na anatarajiwa kuizuru tena Israel.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com