1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden: Kampeni ya Donald Trump ni tishio kwa demokrasia

29 Septemba 2023

Rais wa Marekani amemshambulia mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump, akiitaja kampeni ya rais huyo wa zamani ya "Fanya Marekani Kuwa Kuu Tena" kama vuguvugu la itikadi kali.

https://p.dw.com/p/4WwCD
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Katika hafla maalum ya kumuenzi marehemu seneta John McCain iliofanyika katika jimbo la Arizona, Biden amesema kuwa, ingawa sio Warepublican wote wanaounga mkono kampeni hiyo, chama hicho kinaendeshwa na watu wenye misimamo mikali.

Biden ameongeza kuwa, iwapo ajenda yao ya "Fanya Marekani Kuwa Kuu Tena" itatekelezwa, basi itabadilisha msingi wa taasisi za demokrasia za Marekani.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa, kulinda demokrasia na taasisi za umma ndio vipau mbele vyake katika azma yake ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Hii ni mara ya nne katika mfululizo wa hotuba za rais huyo wa Marekani ambapo amezungumzia juu ya tishio kwa demokrasia, mada ambayo ameifanya muhimu katikati ya kupungua kwa uungwaji mkono wake miongoni mwa wapiga kura.