Beijing. Naibu waziri mkuu China afariki. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Beijing. Naibu waziri mkuu China afariki.

Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kuwa naibu waziri mkuu nchini humo Huang Ju amefariki dunia.

Mshirika mkubwa wa rais wa zamani wa China Jiang Zemin , Huang Ju alipanda ngazi za uongozi katika jimbo la Shanghai na kuingia katika duru za ndani ya uongozi wa chama cha kikomunist nchini humo.

Shirika hilo la habari halikutoa sababu ya kifo cha kiongozi huyo, licha ya kuwa Huang Ju amekuwa mgonjwa, akiwa na saratani ya kongosho, kwa muda wa mwaka mmoja sasa. Alikuwa na umri wa miaka 68.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com