1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustria

Austria yawafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi

Lilian Mtono
14 Machi 2024

Austria imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi na kuwatangaza kuwa wasiotakiwa kuingia tena nchini humo.

https://p.dw.com/p/4dUPB
Austria | Polisi wa Austria
Polisi wa Austria wakiwa katika majukumu yao. Taifa hilo linalosika kwa upelelezi wa kiwango cha juu limewafukuza wanadiplomasia wawili wa UrusiPicha: Imago Images/T. Steinmaurer

Wanadiplomasia hao wamepewa hadi Machi 19 kuondoka nchini humo, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Austria jana Jumatano.

Amesema wanadiplomasia hao wamefanya vitendo visivyoendana na hadhi yao ya kidiplomasia, bila ya kufafanua zaidi.

Watu hao wamekuwa wakifanya kazi katika ubalozi wa Urusi mjini Vienna.

Hatua hii inafanya jumla ya wanadiplomasia wa Urusi waliofukuzwa Austria katika miaka ya karibuni kufikia 11.

Ubalozi wa urusi mjini Vienna umeeleza kughadhabishwa na hatua hiyo, na kusema ni ya kisiasa huku ukiahidi kulipiza kisasi, limearifu shirika la habari la Urusi, TASS.