ANKARRA : Uturuki kuidhinisha kutuma jeshi Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARRA : Uturuki kuidhinisha kutuma jeshi Iraq

Uturuki leo inatazamiwa kukaidi shinikizo la jumuiya ya kimataifa na kuipa kibali vikosi vyake kuingia kaskazini mwa Iraq kutokomeza waasi wa Kikurdi waliopiga kambi huko juu ya kwamba haipi matarajio makubwa kuwepo shambulio hilo kwa uhakika.

Marekani mshirika wa Uturuki katika Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO imesema inafahamu shauku ya Uturuki ya kupambana na waasi wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi cha PKK kilichopigwa marufuku lakini inahofu kwamba kuingia kwa nguvu kwenye eneo hilo kunaweza kuvuruga utulivu katika eneo lenye amani kubwa nchini Iraq na eneo zima kwa jumla.

Idhini ya bunge itaweka msingi wa sheria wa kuchukuliwa kwa hatua ya kijeshi na kulipa uhuru jeshi kuchukuwa hatua inapotaka na inapoona haja hiyo.

Makamo wa rais wa Iraq Tareq al-Hashemi amekuwa akijaribu kumshawishi Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan na Rais Abdullah Gul hapo jana mjini Ankarra kujiepusha na hatua ya kijeshi na kutafuta ufumbuzi wa kidiplomasia.

Al- Hashemi anasema jambo hilo linabidi kufanyika kwa mafahamiano ya pamoja na anafikiri Uturuki iko kwenye hali ngumu kwamba wanafahamu hasira ya wananchi wa Uturuki wasi wasi wa serikali ya Uturuki kuhusiana na harakati za kigaidi kwenye mpaka na wanawahurumia sana.

Erdogan yuko chini ya shinikizo zito la kushambulia makambi ya PKK kaskazini mwa Iraq kufuatia mashambulizi kadhaa ya waasi hao dhidi ya vikosi vya Uturuki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com