Al-Shabaab bado ni tishio kubwa kwa Somalia na nchi jirani
25 Desemba 2025
Matangazo
Kwa mujibu wa ripoti hiyo mnamo mwaka huu, wapiganaji wa Al-Shabab walifanya wastani wa mashambulizi sita kwa mwezi nchini Kenya, hasa katika kaunti za Mandera na Lamu ambazo zinapakana na Somalia.
Ripoti hiyo imeongeza kusema licha ya juhudi za vikosi vya Somalia na vya kimataifa za kuzuia operesheni za kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeda, bado uwezo wa kundi hilo ni mkubwa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura mapema wiki hii na kupitisha kwa kauli moja, azimio la kukiongezea muda kikosi cha Umoja wa Afrika cha askari wa kulinda amani nchini Somalia hadi Desemba 31, mwaka ujao wa 2026.