1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi 9 wa ANC wafa katika ajali Afrika ya Kusini

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Wafuasi 9 wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye mkutano wa kampeni kupata ajali karibu na mji wa Paulpietersbug.

https://p.dw.com/p/4crm4
Afrika Kusini
Moja ya barabara Afrika KusiniPicha: M. Harvey/WILDLIFE/picture alliance /

Wafuasi 9 wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye mkutano wa kampeni kupata ajali karibu na mji wa Paulpietersbug. Kulingana na mamlaka za usalama barabarani nchini humo, jumla ya watu 70 walikuwemo ndani ya basi lililopata ajali na baadhi yao wamejeruhiwa.

Polisi wamesema basi hilo lilipinduka baada ya kupoteza mwelekeo. Watu wanane walikufa papo hapo na mmoja alifariki baadaye baada ya kufikishwa hospitalini. 

Soma habari hii:Takriban watu 20 wafariki katika ajali Afrika Kusini 

Waathiriwa wa tukio hilo ni miongoni mwa maelfu ya watu waliokuwa wamefurika katika uwanja wa mpira mjini Durban Jumamosi katika uzinduzi wa ilani ya uchaguzi wa chama cha ANC.

Afrika Kusini itafanya uchaguzi wa kitaifa na majimbo mnamo Mei 29 mwaka huu.