1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Mahakama: Zuma hastahili kugombea uchaguzi wa Mei

20 Mei 2024

Mahakama ya kikatiba ya Afrika Kusini imetoa hukumu leo Jumatatu kwamba rais wa zamani wa Taifa hilo Jacob Zuma hapaswi kugombea katika uchaguzi wa bunge utakaofanyika wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4g4EV
Rais wa zamani Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani Afrika Kusini Jacob ZumaPicha: AP/picture alliance

Uamuzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu kufuatia uwezekano wa  kuathiri matokeo ya uchaguzi. 

Kesi hiyo imetokana na uamuzi wa mwezi Machi wa Tume ya uchaguzi kumuondowa Zuma katika uchaguzi huo kwa madai kwamba katiba inakataza mtu yoyte aliyetumikia kifungo cha miezi 12 au zaidi kushikilia nafasi ya bunge. 

Mwaka 2021 Zuma alifungwa miaka 15 jela kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake kwa tuhuma za kuhusika na rushwa.

Soma pia:Zuma azindua ilani ya uchaguzi kwa kutoa ahadi lukuki

Mwezi Aprili mahakama ikabatilisha uamuzi wake ikisema kipengee hicho cha katiba kinatumika kwa watu walio na nafasi ya kukata rufaa dhidi ya kesi zao na Zuma hakuwa katika kundi hilo. 

Baadae tume ya uchaguzi ikapeleka kesi hiyo katika mahakama ya kikatiba.