1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 5137 wadaiwa kufa katika maandamano Iran

24 Januari 2026

Zaidi ya vifo 5,137 vimethibitishwa katika wimbi la maandamano makubwa nchini Iran. Haya yameripotiwa leo na shirika la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu nchini Iran lililo na makao yake nchini Marekani (HRANA).

https://p.dw.com/p/57Nae
Iran Teheran 2025 | maandamano
Waandamanaji nchini Iran mnamo Desemba 29,2025Picha: Social Media/ZUMA/IMAGO

Wanaharakati hao wamesema shughuli ya kutathmini na kuthibitisha idadi ya vifo inachukua muda mrefu, na kusema hali hiyo inachangiwa na kuzimwa na kukatizwa kwa mtandao wa intaneti kunakopunguza kasi ya mchakato huo.

Kundi hilo linachunguza visa vingine 12,904, huku watu wengine 7,402 zaidi wakisemekana kujeruhiwa vibaya.

Ripoti rasmi zinaonyesha watu 3,117 walikufa katika ghasia hizo.

Balozi waIran nchini Uswisi amedai kuwa zaidi ya watu 2,400 waliuawa katika shughuli za kigaidi.

Maandamano hayo yaliyochochewa na mzozo mkubwa wa kiuchumi nchini humo, yalizuka mwishoni mwa Disemba.

Wafanyabiashara walikuwa wa kwanza kuingia barabarani namaandamano makubwa yakazuka katika miji mikuu mnamo Januari 8 na 9, kabla ya kukandamizwa kikatili.