1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kwa Waislamu Tanzania kudumisha upendo

Hawa Bihoga22 Agosti 2018

Viongozi wa dini na serikalini wamewataka Waislamu na wananchi wote kuhakikisha kila mmoja analinda amani ya taifa hilo ambayo imejengwa katika misingi ya upendo, amani, kuvumiliana na kuheshimiana.

https://p.dw.com/p/33YlZ
China Hui-Chinesen in Peking | Eid al-Fitr
Picha: Getty Images/K. Frayer

Waislamu kote nchini Tanzania wametakiwa kudumisha upendo miongoni mwao pamoja na kuheshimu mamlaka zilizopo, ili kuenzi mafundisho ya kiongozi wa dini hiyo mtume Muhammad S. A W. Hayo yamesemwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, katika kutekeleza ibada ya Eid ul -Hajji inayotekelezwa baada ya kumalizika ibada ya Hijja katika miji wa Makka na Madina.

Ibada ya Hija ambayo ni nguzo ya tano katika dini ya Kiislamu, hutekelezwa katika mji wa Maka na Madina kwa waislamu walio na uwezo hukamilishwa kwa ibada maalum ya sala ya Eid na kisha hufuatiwa na zoezi la kuchinja.

Kwa nchini Tanzania swala hii imetekelezwa kitaifa katika viwanja vya msikate tamaa vingunguti mjini dar es salaam, ambapo waumini wa dini hiyo wametakiwa kuhakikisha wanaenzi mafunzo ya kiongozi wa dini hiyo mtume Muhammad S.A.W, ambae mbali na mambo mengine lakini pia ameelekeza mapenzi ndani ya jamii, kuwakumbuka maskini na faqir, kuheshimu wazazi pamoja na mamlaka zilizopo pamoja na kuwakumbuka watu wasiojiweza ndani ya jamii ili kuondoa matabaka.

Wito wa upendo

Kaimu shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam Hassan Mwinyipingu aliuambia umma huo kuwa, inamlazimu kila mmoja kwa nafasi yake kuonesha mapenzi kwa mwingine wakiwemo wazazi.

Ibada ya Eid ul -Hajji inayotekelezwa baada ya kumalizika ibada ya Hijja katika miji wa Makka na Madina na sherehe ya Eid huhusishwa na kuwachinja wanyama ambapo jamaa, marafiki na watu wasiojiweza pia hupewa kama chakula
Ibada ya Eid ul -Hajji inayotekelezwa baada ya kumalizika ibada ya Hijja katika miji wa Makka na Madina na sherehe ya Eid huhusishwa na kuwachinja wanyama ambapo jamaa, marafiki na watu wasiojiweza pia hupewa kama chakulaPicha: Reuters/F. Mahmood

Mara baada vya swala hiyo ilifuatiwa na baraza la Eid katika viwanjwa hivyo iliofunguliwa kwa usomaji wa Qur-an tukufu Surat Hijja.

Katika baraza hilo lililohudhuriwa na viongozi wa kitaifa katika dini, serikali na hata vyama vya siasa, mgeni rasmi waziri wa ulinzi nchini akitoa salamu za rais magufuli, amewataka wananchi wote kuhakikisha kuwa kila mmoja kwa nafasi yake analinda amani ya taifa hilo alilolitaja limejengwa katika misingi ya upendo, amani kuvumiliana na kuheshimiana.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kaimu mufti wa Tanzania shekhe Masoud Jongo amesema kuwa, dini ya kiislamu inaendeshwa katika misingi ya rejea ya qur-an tukufu, pamoja na sunnah za mtume Muhammad s.a.w, na si kwa maoni au mtazamo wa mtu mmoja mmoja au kundi fulani.

Nao baadhi ya waislamu waliofanikiwa kutekeleza ibada hiyo ya Eid wamesema kuwa, kwa wale walio na uwezo ambao tayari wameshafanya Hija ni vyema wakatoa ufadhili kwa waumini wengine ili waweze kutekeleza ibada hiyo ambayo inatakiwa kufanywa na kila mmoja ispokuwa uwezo husalia kuwa kikwazo.

Mwandishi: Hawa Bihoga
Mhariri:Josephat Charo