WHO Yapunguza Idadi ya Washukiwa wa Ebola Afrika ya Kati
2 Juni 2026
WHO imesema hadi Mei 31, jumla ya visa 321 vimethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vikiwemo vifo 48, huku Ugandaikiripoti visa 9 vilivyothibitishwa na kifo kimoja.
Msemaji wa WHO, Christian Lindmeier, alieleza kuwa kupungua kwa visa vinavyoshukiwa kunatokana na uchunguzi zaidi ulioonesha wengi wa wagonjwa walikuwa na magonjwa mengine kama malaria au homa ya uti wa mgongo.
Alisisitiza kuwa mtu yeyote mwenye dalili zinazofanana na Ebola huorodheshwa kama mshukiwa hadi vipimo vitakapothibitisha.
Mlipuko huo ulitangazwa rasmi Mei 15 katika jimbo la Ituri, mashariki mwa DRC, ingawa unaaminika ulikuwepo kabla ya hapo.
Hadi sasa, hakuna chanjo wala tiba maalum ya kirusi cha aina ya Bundibugyo, hivyo juhudi zinaelekezwa zaidi katika kujikinga na kudhibiti maambukizi.