1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock ambebesha dhamana Putin kuhusu vita vya Ukraine

Saumu Mwasimba
21 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amezikumbusha nchi tajiri kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi duniani G20, kwamba rais Vladimir Putin anabeba dhamana ya athari zinazotokana na vita vya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cgS3
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Kira Hofmann/photothek/IMAGO

Annalena Baerbock ameyasema hayo jana Jumanne kabla ya kuelekea nchini Brazil kushiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi hilo.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Ujerumani ameongeza kusema kwamba hawatoitelekeza misingi ya Umoja wa Mataifa na wataendelea kusimama imara na Ukraine mpaka watu wa nchi hiyo watakapoishi kwa amani na uhuru kwa mara nyingine.

Mkutano wa G20 utakaohudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Rio de Jeneiro unaoanza leo utajadili kuhusu vita nchini Ukraine, Gaza na kitisho cha kusambaa vita hivyo Mashariki ya Kati.

Mkutano huo utamalizika kesho Alhamisi.