SiasaUfaransa
Lecornu anusurika kura za kutokuwa na imani bungeni
16 Oktoba 2025
Matangazo
Siku ya Jumatano, Lecornu alitangaza kusitisha muswada wa mageuzi ya pensheni unaopingwa vikali na watu wengi na ambao ulitakiwa kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64, hatua iliyomuwezesha Lecornu kupata uungwaji mkono wa chama cha kisoshalisti.
Kunusurika kwa Lecornu na kura hizo za kutokuwa na imani naye, kunaipa fursa serikali yake kuendelea na kazi ngumu ya kujaribu kupitisha bajeti ya mwaka ujao ambayo inajumuisha hatua za kubana matumizi na kodi mpya. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitishia kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa Bunge wa mapema iwapo serekali ya Lecornu ingeliangushwa.