Watu 98 washtakiwa kwa uhaini nchini Tanzania
7 Novemba 2025
Matangazo
Nyaraka hizo katika mahakama ya hakimu mkaazi Dar es Salaam, zimesema kuwa washtakiwa walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa madhumuni ya kuitisha mamlaka ya nchi hiyo na kusababisha uharibifu wa mali za serikali.
Hata hivyo, hakukuwa na ufafanuzi wa tuhuma maalum dhidi ya washtakiwa hao isipokuwa kwa mfanyabiashara mmoja mwanamke ambaye ameshtumiwa kwa kuwahimiza watu kununua barakoa za kujikinga na gesi za machozi kutoka kwa biashara yake wakati wa maandamano hayo.
Rais wa chama kikuu cha wanasheria nchini Tanzania, Boniface Mwabukusi, amesema hadhani kama washtakiwa hao waliwakilishwa na wakili.
Serikali haijajibu ombi la tamko kuhusu hali hiyo.