1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUrusi

Zaidi ya watu 60 wauawa kwenye tamasha la muziki Moscow

23 Machi 2024

Idara ya usalama ya Urusi imesema zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia tamasha la muziki lililofanyika karibu na mji mkuu Moscow.

https://p.dw.com/p/4e35t
Kikosi cha oparesheni maalum wa Urusi wakishika doria katika ukumbi wa Crocus kulikofanyika tamasha la muziki
Kikosi cha oparesheni maalum wa Urusi wakishika doria katika ukumbi wa Crocus kulikofanyika tamasha la muzikiPicha: Sergei Vedyashkin/Moscow News Agency/REUTERS

Watoto watano wameripotiwa kuwa miongoni mwa majeruhi waliopelekwa hospitali.

Takriban washambuliaji watano waliokuwa wameficha nyuso zao walifyatua risasi kwa watu waliokuwa wakihudhuria tamasha lililofanyika kwenye ukumbi wa Crocus, katika kitongoji cha kaskazini magharibi cha Krasnogorsk.

Soma pia: Kremlin kwa mara ya kwanza yaitaja operesheni ya Ukraine kuwa vita

Ukumbi huo wa Crocus wenye uwezo wa kubeba watu 6,200 ulikuwa unaanda tamasha la muziki wa Rock.

Shambulio hilo linatajwa kuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi nchini Urusi tangu kuvamiwa kwa shule ya Beslan mnamo mwaka 2004 ambapo zaidi ya watu 330, nusu kati yao wakiwa watoto, waliuawa.