WASHINGTON : Rais Bush akutana na Dalai Lama | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Rais Bush akutana na Dalai Lama

Rais George W. Bush wa Marekani amekutana kwa faragha na Dalai Lama ikiwa ni siku moja kabla ya kutunukia rasmi kwa tuzo ya Marekani kiongozi huyo wa kidini wa Tibet.

China imeonya kwamba mipango ya Marekani kumtunuku Medali ya Dhahabu ya Bunge la Marekani Dalai Lama inaweza kuathiri uhusiano kati ya China na Marekani.Utawala wa Bush haukupa hadhi kubwa mkutano huo wa Bush na Dalai Lama katika jaribio la kuituliza China.

Iwapo Bush atahudhuria sherehe za kutunukiwa tuzo kwenye bunge la Marekani itakuwa ni mara ya kwanza kwa rais aliyeko madarakani kuonekana hadharani akiwa pamoja na Dalai Lama mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel ambaye China inamuona kuwa ni muasi anayetaka kulitenga jimbo la Tibet na ni mhaini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com