1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina kesho kuadhimisha miaka 76 kufurushwa

Saumu Mwasimba
14 Mei 2024

Wapalestina kesho Jumatano, wataadhimisha kumbukumbu ya miaka 76 tangu walipofurushwa kwenye ardhi yao ambayo hivi sasa ni kile kinachojulikana kama Israel.

https://p.dw.com/p/4fqll
Wakimbizi wa Palestina 1948
Wakati wa vita vya 1948 iliyozusha ukimbizi katika kile kilichofahamika kama 'Nakba,' au janga.Picha: ELDAN DAVID/EPA/dpa/picture-alliance

Takriban Wapalestina 700,000 walikimbia au kuondolewa kwa nguvu kwenye makaazi yao kabla na wakati wa vita vya mwaka 1948 kati ya Waarabu na Israel vilivyofuatia kuundwa kwa dola la Israel,katika kile kinachoitwa na Wapalestina kuwa Janga au Nakba.

Baada ya vita hivyo Israel ilikataa kuwaruhusu Wapalestina kurudi nyumbani na hatua hiyo imekuwa ikisababisha kilio kikubwa cha Wapaletina katika mgogoro baina ya pande hizo mbili.

Kuna kiasi Wapalestina milioni 6 wanaoishi nje ya ardhi yao,wengi wakiwa kwenyemakambi ya wakimbizi katika mataifa ya Lebanon,Syria,Jordan na Ukingo wa Magharibi kunakokaliwa na Israel.