1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wakimbizi 150 wa Rohingya wawasili Indonesia

Sudi Mnette
1 Januari 2024

Takriban wakimbizi 150 wa Rohingya, wengi wao wakiwa wanakabiliwa na njaa, wanawake na watoto dhaifu, wamewasili katika eneo la ufuo wa Indonesia Jimbo la Sumatra Kaskazini baada ya wiki kadhaa baharini.

https://p.dw.com/p/4akfc
Asia Top Shot 2023 | Indonesien I Ankunft von Rohingya-Muslimen in Pidie, Aceh
Picha: Rahmat Mirza/AP/picture alliance

Taarifa za jana Jumapili za maafisa katika eneo hilo inasema kundi la wanaume 53, wanawake 39 na watoto 55 waliwasili Karang Gadih eneo la pwani katika wilaya ya Langkat. Watano kati ya wakimbizi walifika wakiwa wagonjwa baada ya safari ndefu na wakazi waliwasaidia kwa kuwapa chakula na maji huku wakisubiri maelekezo kutoka kwa idara ya uhamiaji na maafisa wa serikali kuamua mahali ambapo wanaweza kuhifadhiwa.Takriban Warohingya 740,000 wamepewa makazi mapya nchini Bangladesh baada ya kukimbia nyumba zao nchini Myanmar kwa kuepuka kampeni ya kikatili ya kukabiliana na waasi ya vikosi vya usalama.