1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa wito kuokolewa Warohingya 185 bahari ya Hindi

24 Desemba 2023

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa haraka wa kuwaokoa watu wapatao 185, wengi wakiwa ni wanawake na watoto ambao wako kwenye mashua karibu na visiwa vya Andaman na Nicobar katika bahari ya Hindi.

https://p.dw.com/p/4aXYZ
Indonesia I Wakimbizi wa Rohingya wakishuka katika mashua.
Wakimbizi wa Rohingya wakitoka kwenye mashua baada ya kuwasili IndonesiaPicha: Rahmat Mirza/AP/picture alliance

Msemaji wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Babar Baloch, alisema walio katika mashua hiyo ni wakimbizi wa Rohingya takriban 70 kati yao ni watoto na 88 ni wanawake na kuongeza kuwa kadhaa kati yao wanahofiwa kuwa katika hali mbaya huku mmoja akiripotiwa kufariki.

Maelfu ya Warohingya ambao wengi wao ni Waislamu na wanaopitia mateso makubwa nchini Myanmar, wanafanya safari hatari za baharini kutoka Myanmar na kambi za wakimbizi nchini Bangladesh kila mwaka wakijaribu kuelekea Malaysia ama Indonesia.

Soma pia:Takriban Warohingya 170 wamewasili Indonesia

Kwa mujibu wa UNHCR tangu mwaka uliopita zaidi ya watu 570, wakiwemo wakimbizi wa Rohingya, wameripotiwa kufariki au kupotea baharini katika safari hizo.