1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 21 wakiwemo watoto 5 wafa katika bahari ya Aegean

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Takribani wahamiaji 21, wakiwemo watoto watano wamekufa baada ya meli kuzama katika pwani ya Uturuki. Maafisa wanasema watu wawili wameokolewa na walinzi wa pwani wa Uturuki.

https://p.dw.com/p/4dghm
Aegean
Wahamiaji 21 wakiwemo watoto 5 wafa katika bahari ya AegeanPicha: Panagiotis Balaskas/AP Photo/picture alliance

Mtu mmoja alifanikiwa kujiokoa mwenyewe. Boti hiyo ilizama kwenye kisiwa kikubwa cha Uturuki cha Gokceada au Imbros kinachopatikana kwenye jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Bahari ya Aegean la Canakkale. 

Juhudi za uokoaji zinafanyika kwa msaada wa ndege moja, helkopita mbili, droni moja, boti 18 na maafisa wapatao 502. Uturuki inawahifadhi wakimbizi karibu milioni 4, wengi ni kutoka Syria.

Serikali mjini Ankara ilifikia makubaliano ya kupewa usaidizi wa kifedha na Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2016 ili kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.