1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina Ulaya kumuidhinisha von der Leyen muhula wa pili

7 Machi 2024

Chama cha European People's, EPP, katika Bunge la Ulaya, kinajiandaa kumuunga mkono rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen, kuwania muhula wa pili wa uongozi kwenye chombo hicho chenye nguvu barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4dFej
Ursula von der Leyen ni waziri wa zamani wa ulinzi Ujerumani
Von der Leyen amehudumu kwa miaka mitano kama mkuu wa Halmashauri Kuu ya UlayaPicha: Yves Herman/REUTERS

Von der Leyen, ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi wa Ujerumani, ameiongoza Halmshauri hiyo kwa miaka mitano, kupitia kipindi cha janga la UVIKO-19, uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwaka 2022 na kipindi cha changamoto ya nishati barani Ulaya.

Akiwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo, alishuhudia Uingereza pia ikijiondoa katika Umoja wa Ulaya,  kuweka sheria mpya za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na mazingira na kuiongoza Ulaya kujikwamua kiuchumi kutokana na janga la korona.

Iwapo atachaguliwa tena na viongozi wote 27 wanaounda Umoja huo, von der Leyen atakuwa na muhula mwengine wa kuisimamia halmashauri hiyo katika sera zake kwenye masuala ya teknolojia, ufadhili wa nchi, usimamizi wa uwekezaji wa China na vikwazo dhidi ya Urusi.