1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Waasi wa Yemen waapa kuendelea kuzamisha meli za Uingereza

3 Machi 2024

Wahouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran wameapa kuendelea kulenga meli za Uingereza katika Ghuba ya Aden.

https://p.dw.com/p/4d7Sv
Waasi wa Kihouthi wa Yemen wameapa kuendelea kuzamisha meli za Uingereza
Waasi wa Kihouthi wa Yemen wameapa kuendelea kuzamisha meli za UingerezaPicha: CENTCOM/Anadolu/picture alliance

Jana Jumamosi Jeshi la Marekani lilithibitisha kwamba meli ya Rubymar inayomilikiwa na Uingereza ilizama baada ya kushambuliwa kwa kombora la masafa marefu lililofyatuliwa na waasi wa Kihouthi wa Yemen mnamo Februari 18.

Kupitia mtandao wa X, naibu waziri wa mambo ya nje katika serikali inayoongozwa na Wahouthi, Hussein al-Ezzi, amesema "Yemen itaendelea kuzamisha meli zaidi za Uingereza, na madhara mengine yoyote yanapaswa kuwa lawama kwa Uingereza,"

Wanamgambo wa Houthi mara kwa mara wamekuwa wakifanya mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya usafirishaji wa biashara wa kimataifa tangu katikati ya Novemba, wakisema wanafanya kazi kwa mshikamano na Wapalestina dhidi ya hatua za kijeshi za Israel huko Gaza.