1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamerhe kuondolewa katika nafasi ya Spika wa Bunge la DRC ?

18 Septemba 2025

Taratibu zinazolenga kumfuta kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Vital Kamerhe zinaendelea huku kukishuhudiwa hali ya mfarakano kati ya rais Félix Tshisekedi na mshirika wake huyo wa zamani.

https://p.dw.com/p/50eLA
Kinshasa | Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Vital Kamerhe
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Vital Kamerhe akizungumza na wafuasi wa "Union Sacrée" mjini Kinshasa: 29.04.2023Picha: Arsene Mpiana/AFP

Kamerhe anakabiliwa na uwezekano huo wa kuondolewa katika wadhifa huo akituhumiwa kwa usimamizi usio na uwazi wa fedha za umma, uongozi mbaya na kupuuza hoja za wabunge wa kitaifa.

Vital Kamerhe  na Félix Tshisekedi waliimarisha ushirikiano wao mjini Nairobi walipounda muungano wao kwa ajili ya mabadiliko baada ya kusaliti makubaliano ya Geneva waliyosaini pamoja na viongozi watano wa upinzani, wakimteua Martin Fayulu kama mgombea pekee katika uchaguzi wa rais wa Desemba mwaka 2018.